31 Julai 2026 - 22:43
Mhadhiri wa Sala ya Ijumaa Tehran: Makombora na Diplomasia Vimeimarisha Mizani ya Nguvu kwa Manufaa ya Iran

Mhadhiri / Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema uwezo wa makombora ya Iran pamoja na diplomasia madhubuti ndivyo vilivyoimarisha mizani ya nguvu kwa manufaa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, huku akisisitiza umuhimu wa kulinda mshikamano wa kitaifa na kuimarisha imani ya wananchi.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Mhadhiri wa Sala ya Ijumaa wa Tehran, Hujjatul Islam wal-Muslimin Mohammad Hassan Abu Torabi Fard, amesema kuwa uwezo mkubwa wa makombora ya Iran pamoja na juhudi za kidiplomasia umeifanya mizani ya nguvu kubaki kwa manufaa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Akihutubia waumini katika Sala ya Ijumaa mjini Tehran, Abu Torabi Fard alisema kuwa nguvu hizo ndizo zinazozima vitisho vya kijeshi vya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, huku mafanikio yaliyopatikana katika medani ya kijeshi yakigeuzwa kuwa mafanikio ya kisiasa kupitia meza ya mazungumzo ya kidiplomasia.

Alieleza kuwa mustakabali wa Iran ni wenye matumaini makubwa iwapo taifa hilo litaendelea kulinda mafanikio yake ya sasa kwa umoja, umakini, uthabiti na mshikamano wa wananchi.

Mhadhiri huyo alisisitiza kuwa ushindi katika medani ya mapambano haupatikani kwa uwezo wa kijeshi pekee, bali pia unategemea uimara wa uwezo wa kujihami, kiwango cha kuzuia mashambulizi ya adui, mshikamano wa kitaifa, mtaji wa kijamii na imani ya wananchi kwa viongozi wao. Alisema mambo hayo yanapaswa kuhifadhiwa na kuimarishwa kwa pamoja ili kuhakikisha usalama na maendeleo ya taifa.

Aidha, Abu Torabi Fard alidai kuwa mkakati mkuu wa maadui wa Iran ni kudhoofisha mtaji wa kijamii kwa kuchochea migawanyiko ya kijamii na kisiasa pamoja na kupunguza imani ya wananchi kwa viongozi wao. 

Alisisitiza kuwa kudumisha umoja wa kitaifa ni nguzo muhimu ya kulinda mafanikio ya Iran na kukabiliana na changamoto za nje.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha